Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi hii, dau la Pogba halikamatiki kumng’oa Man United lazima ujipange, Badiashile, Lukaku sokoni

Manchester United wameongeza dau la pauni milio 30 juu ya thamani ya kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 26, na sasa wanataka dau la £180m kumuuza mchezaji huyo waliyemnunua kwa dau la £89m in 2016.(Star)
Pogba
Juventus wamesitisha hamu yao ya kutaka kumsajili Pogba, wakitoa fursa kwa Real Madrid kumsaini mchezaji huyo wa Ufaransa. (Mail)
Manchester United huenda ikamsajili beki wa Monaco na Ufaransa 19 Benoit Badiashile,ambaye pia anawaniwa na Wolves – iwapo watamkosa beki a leicester na Uingereza Harry Maguire, 26. (L’Equipe, via Express)Harry Maguire
Inter Milan huenda wakalazimika kulipa takriban £90m ili kuweza kuwa na fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji na Man United Romelu Lukaku, 26, msimu huu (Telegraph)
Arsenal itataka kulipwa dau la £8.8m ili kumuuza nahodha wake na beki wa Ufaransa Laurent Koscielny, 33 ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo na alikataa kuondoka na wenzake kuelekea Marekani kwa mechi za maandilizi ya msimu ujao. (London Evening Standard)
Arsenal imeimarisha hamu yake ya kumsaini beki wa Benfica na Ureno Ruben Dias, 22, kufautia maamuzi ya hivi karibuni yaKoscielny . (Mail)Laurent Kolscienly
West Ham infanya mazungumzo na Eintracht Frankfurt over a deal to sign 25-year-old French striker Sebastian Haller for around £40m. (Sky Sports)
Mshambulaji wa Manchester United na Jamhuri ya Ireland Mipo Odubeko, 16, ambaye aliifungia magoli 35 shule yake ya mafunzo ya soka msimu uliopita amekataa kuongeza kandarasi mpya.. (Mail)
Juventus imekubali dau la £63m kumnunua beki wa Ajax na Uholanzi Matthijs de Ligt mwenye umri wa miaka 19. (De Telegraaf – in Dutch)Pedro Obiang
West Ham wametaka kulipwa kitita cha £10m ili kumsajiuli kiungo wa kati wa Equatorial Guinea Pedro Obiang, 27, licha ya klabu za Itali kama vile Bologna na Sassuolo kuonyesha hamu ya kumnunua mchezaji huyo. (Sun)
Tottenham inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Leeds na Uingereza Kalvin Phillips, ambaye klabu hiyo ya York Shire inasema ana thamani ya £30m. (Mirror)
Manchester United bado ina hamu ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle na Uingereza Sean Longstaff kutoka Newcastle licha ya klabu hiyo kutokubaliana juu thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)
Lakini bei ya Newcastle ya £50m inaweza kuilazimu United kumaliza hamu yao.. (ESPN)

TETESI ZA SOKA ALHAMISIAntoine Griezmann

Barcelona inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa na Atletico Madrid Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid kwa dau la £107m . (Mirror)
Duru kutoka Barcelona zimekana ripoti kwamba tayari klabu hiyo imetoa dau hilo (Sport)
Mshambuliaji Gareth Bale, 29, alishiriki mazoezi na wenzake wa Real Madrid nchini Canada huku akiendelea kujilazimisha katika mipango ya mkufunzi Zinedine Zidane. (Mail)Gareth Bale
Newcastle inajiandaa kumteua mkufunzi wa Sheffield Wednesday Steve Bruce kuwa kocha wake na wanatumai ataweza kujiunga na timu hiyo katika maandalizi ya msimu ujao ziarani China. (Telegraph)
Newcastle inajadiliana kuhusu fidia ya takriban £5m na klabu ya Sheffield Wednesday ili kumsajili Bruce. (Times)
Manchester United na Manchester City zimepigwa jeki katika harakati za kumsajili Bruno Fernandes huku klabu yake ya Sporting Lisbon ikikaribia kumsajili mchezaji atakayechukua mahala pake.. (Mirror)
Lukaku
Manchester United imeanza majadiliano na Roma kuhusu kumuuza mshambuliaji wake mwenye umri wa miaka 26 Romelu Lukaku. (Goal.com)
Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Inter Milan Piero Ausilio amesafiri kuelekea mjini London ili kukutana Manchester United ili kuona iwapo dau watakaloliwakilisha kumsajili Lukaku litafanikiwa kumnunua (Guardian)
Ajenti wa beki wa Tottenham Toby Alderweireld amefanya mazungumzo na Roma kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 mwenye thamani ya £22.5m. (Calciomercato)Toby Alderweireld
Mchezaji wa Real Madrid na Jamhuri ya Dominican Mariano Diaz, 25, hana hamu ya kujiunga na Arsenal msimu huu. (AS, via Mirror)
Paris St-Germain wanatarajiwa kuimarisha hamu yao ya kutaka kumsajili mchezaji wa Everton Idrissa Gueye kwa dau la £27m kwa kiungo huyo wa Senegalr. (L’Equipe, via Sun)
Arsenal ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Real Madrid’s Dani Ceballos kwa mkopo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 pia amekuwa akifanya mazungumzo na klabu ya Tottenham. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anatarajiwa kuzuia jaribio la Steven Gerrard kumrudisha winga Ryan Kent katika klabu ya Rangers msimu huu. Mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 22 alihudumu msimu uliopita kwa mkopo na klabu hiyo ya Uskochi.. (Express)Steven Bergwijn
Ajenti wa winga wa PSV Eindhoven Steven Bergwijn, 21, ameiambia klabu ya Bayern Munich kwamba mteja wao anayekumbwa na uvumi wa kuhamia klabu ya Manchester United yuko tayari kuhamia Ujerumani. (Express)
Manchester United wamefutilia mbali hamu yao inayoripotiwa ya kumsaini mchezaji wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25, ambaye amehusishwa na Arsenal. (Manchester Evening News)
Mshambuliaji wa Bournemouth na Uingereza Callum Wilson, 27 – anayelengwa na West Ham – anatarajia kutia saini mkataba mpya wa miaka minne na The Cherries. (Talksport)Peter Crouch
Bournemouth inajiandaa kumruhusu mchezaji mwenye umri wa miaka 25 winga wa Uskochi Ryan Fraser, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Arsenal, kuondoka kwa dau la bila malipo mwisho wa msimu ujao badala ya kumuuza msimu huu. (Express)
Mchezaji wa zamani wa Uingereza Peter Crouch, 38, hajaamua iwapo atastaafu baada ya kandarasi yake na Burnley kuisha msimu huu . (Talksport)
Wachezaji wanaolengwa na Newcastle Joelinton, mchezaji wa Hoffenheim ,22 raia wa Brazil pia ananyatiwa na Wolves. (Newcastle Chronicle)
Winga wa Crystal Palace 26 Wilfried Zaha, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal hakushirikishwa katika picha za jezi mpya ya ugenini ya klabu hiyo. (Express)

Post a Comment

0 Comments