Rais wa Uturuki azungumza na  Khan kuhusu Jammu & Kashmir

 

Rais wa Uturuki azungumza na waziri mkuu wa Pakistan kuhusu Jammu & Kashmir.
Recep Tayyıp Erdoğan azungumza na waziri mkuu wa Pakistani Imran Khan  kwa njia ya simu  kuhusu  matukio ya hivi karibuni kati ya India  na Pakistani  katika eneo la Jammu & Kashmir.
Taarifa kutoka ikulu mjini Ankara katika kitengo kinachohusika na upashaji habari zimesema kwa waziri mkuu wa Pakistani Imran Khan amempigia simu rais Erdoğan na kumpa taarifa kuhusu hali inayoendelea  katika eneo la Jammu & Kashmir.
Katika mazungumzo yao  rais wa Uturuki na waziri mkuu huyo wa Pakistani, rais Erdoğan amekumbusha  umuhimu wa mazungumzo na kutoa wito kwa pande zote mbili  kuweka mbele mazungumzo.
India imeondoa makubaliano ya eneo la Jammu & Kashmir makubaliano ya zaidi ya nusu karne na kfungu cha sharia  nambari 370 cha katiba.
  imeandaliwa na Nadhiri .A.Rashidi

Post a Comment

0 Comments