Ronaldo aweka rekodi nyingine kubwa duniani, Abakiza magoli 57 kumvua Pelé ufalme wa soka

 Mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo jana usiku ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tano wa muda wote duniani kufikisha magoli 700.

by Neezy

 

Goli la 700 la Cristiano Ronaldo amefunga usiku wa kuamkia leo Jumanne Oktoba 15, 2019 dhidi ya Ukraine kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya Euro.
Kwa rekodi hiyo, Ronaldo anakuwa mchezaji wa 5 kufikisha magoli 700 akiwa nyuma ya Pele mwenye magoli 757, Josef Bican goli 756, Romario goli 749, Ferenc Puscas 704.

 

Na klabu alizotupia magoli hayo ni Sporting Lisbon 5 , Manchester United 118,  Real Madrid 450, Juventus 32 na Ureno magoli 95.
Kwa sasa Ronaldo amebakisha magoli 57 kuvunja rekodi iliyodumu muda mrefu mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil,  Pele ya magoli 757.


Post a Comment

0 Comments