Marioo awagonganisha Diamond na Harmonize


by Nadhiri

                                    Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Fleva Marioo inasemekana kuwaingiza kwenye vita mpya, Diamond Platnumz na Harmonize baada ya kila mmoja kutamani kufanya nae kazi.
Marioo, kijana anayetajwa kuwa ‘moto’ kwa mwaka huu wa 2020, anawaingiza Diamond au Mondi na Harmonize au Harmo kwenye vita ya kumgombea kwani wote wanatajwa kuiwania saini yake.
Suala hilo lilianza kuibuka katika mitandao ya kijamii baada ya kusambaa picha za mwanamuziki huyo akiwa na Diamond Platnumze huku picha nyingine akiwa na Harmonize jambo lilianza kujadili na wadau wa muziki.
Picha hizo zilizosambaa ziliwaonesha Diamondi akiwa na Marioo walipokutana jijini Lagos nchini Nigeria kwenye Tuzo za Sound City ambapo wawili hao walikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa wakiziwania tuzo hizo.
Picha hizo mbalimbali ziliwaonesha wawili hapo kuwa na ukaribu mkubwa kushibisha hoja za kwamba, huenda bwa’mdogo huyo yupo kwenye harakati za kusainiwa na lebo hiyo kubwa nchini.
Mashabiki wa Harmonize walisema, msanii wao ana akili kubwa na ndiyo maana hata hao Wasafi wanahaha kutafuta mtu wa kuziba pengo lake ambaye aliachana na Wasafi mwishoni mwa mwaka jana.

Hila hadi sasa hakuna taarifa yoyo kuhusu mwanamuziki huyo anachukuliwa na upande gani japokuwa kila sehemu inataka kufanya nae kazi kutokana na ubora wa kuimba wa mwanamuziki huyo wa Bongo Fleva.