Breaking News: Kenya yathibitisha Mgonjwa wa kwanza wa Corona

Serikali ya Kenya hii leo siku ya Ijumaa imethibitisha mgonjwa wa kwanza mwenye virusi vya Corona.
Waziri wa afya nchini humo Mutahi Kagwe amesema mgonjwa huyo wa kike aliingia nchini Kenya akitokea Marekani kupitia Uingereza.

Kangwe amesema mgonjwa huyo tayari ameanza kupatiwa matibabu na kuwasihi Wakenya kubaki watulivu.
Hata hivyo ameongeza kuwa mgonjwa hiyo anaendelea vivuri, ana kula na hatatolewa kutoka hospitali mpaka atakapothibitika amepona.
Mwanamke huyo kwa sasa yupo Kenyatta National Hospital’s Infectious Disease Unit, huku serikali ikisema kuwa imefuatilia mawasiliano yake yote ambayo mgonjwa huyo amefanya tangu kuingia nchini.
Kwa mujibu wa Daily Nation, Kenya imevunja safari zote za nje ya nchi hiyo isipokuwa zile za lazima.

Post a Comment

0 Comments