Corona: Zanzibar Yafunga Baa “Ukiingia Tunakuweka Karantini”

Waziri wa Afya wa ZanzibarHamad Rashid Mohamed amesema serikali imewaweka karantini wananchi 65 wakiwemo vigogo wa serikali na maofisa sita wa afya kwa ajili ya uchunguzi wa virusi vya Corona.

Serikali imewataka watu wote wanaokwenda sokoni kufanya manunuzi na kuondoka haraka badala ya kugeuza soko kuwa sehemu ya mazungumzo na ukomo wa muda wa masoko ni saa 12 jioni.

Aidha, imepiga marufuku mikusanyiko yote inayokutanisha watu wengi kwa pamoja ikiwemo Michezo, harusi, warsha, sherehe za kifamilia na mikutano. Wakuu wa Mikoa wametakiwa kusimamia utekelezaji wa maagizo haya.

Post a Comment

0 Comments