Coronavirus: Rwanda yatangaza kisa chake cha kwanza cha virusi vya Corona (COVID-19)Rwanda imethibitisha kisa chake cha kwanza cha virusi vya Corona (COVID-19). Mgonjwa huyo ni raia wa India aliyewasili Rwanda Machi 8 kutoka Mumbai, India, kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya afya.
Raia huyo hakuwa na dalili zozote za virusi vya Corona wakati anawasili nchini Rwanda na alijipeleka mwenyewe kwenye kituo cha afya Machi 13, ambapo alifanyiwa vipimo mara moja.
Wizara ya afya imesema kwa sasa anaendelea na matibabu, hali yake imeimarika na ametengwa na wagonjwa wengine.
Wote aliotangamana na mgonjwa huyo wanaendelea kutafutwa katika juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo.
''Raia wote wa Rwanda wanastahili kufuata sheria zote zilizotolewa na wizara ya afya hasa kuhusu kuosha mikono kila mara,'' taarifa hiyo imesema.
Kagame asema Rwanda iko tayari kukabialiana na janga la Corona
Kupitia ujumbe wake katika mtandao wa Twitter, Rais Paul Kagame amesema, '' Kama kawaida tutapita changamoto hizi kupitia ushirkiano.''
Alitaka raia kufikiria waathirika, familia zao na rafiki zao.''
Bwana Kagame amewatakia wagonjwa wote afueni ya haraka na kumshukuru Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkuu wa Shirika la Afya Duniani la Umoja wa Mataifa (WHO), na idara yote kwa ujumla kwa uongozi wao wakati huu wa majaribu na kuwaombea wahudumu wa afya kuendelea kuwa imara wanapokuwa mstari wa mbele kukabiliana na janga hili.
 • Kenya na Ethiopia zatangaza kisa cha kwanza cha virusi vya corona
 • Je juhudi za kutafuta chanjo ya coronavirus zimefika wapi?
 • Marufuku kupeana mikono, busu katika nchi hizi
 • Dr Ngamije Daniel, Minisitiri w'ubuzima w'u Rwanda, avuga ko igihugu cyiteguye
 • Taarifa hiyo pia imesihi raia kutohudhuria mikusanyko ya umma na kuarifu mamlaka iwapo watashuhudia tukio wanalolishuku kupiga simu kupitia nambari 114.
  Kupitia mahojiano na kituo cha redio cha taifa cha Radio Rwanda, Dr Ngamije Daniel, Waziri wa Afya wa Rwanda amesema kwamba nchi yake iko tayari kupambana na virusi hivyo.
  ''Nchi iko tayari ... kwa misingi wafanyakazi wenye ujuzi...''
  Waziri Dr Ngamije pia amesema kwamba katika kipindi cha wiki mbili zijazo kuanzia Jumamosi, mikusanyiko ambayo sio lazima au makutano yoyote ya watu imepigwa marufuku.
  Aidha, shirika la ndege la Rwanda limetangaza kusitisha safari zake za ndege kwa muda kwena nchini India kwasababu ya mlipuko wa Corona hadi Aprili 30, 2020 na kuahidi kwamba aitachukua hatua kadhaa kwa safariki walioathirika kama kubadilisha safari zao bila malipo ya ziada au hata kuwarejeshea pesa zao walioathirika.
 • Mhudumu wa afya
 • Nchi zingine zilizothibitisha mgonjwa wa virusi vya Corona
  Wakati huohuo, Sudan imesema mwanamume aliyekuwa na umri wa miaka ya 50 na kuaga dunia Alhamisi katika mji mkuu wa Khartoum alikuwa na virusi vya Corona.
  Mwanamume huyo alikuwa ametembelea Falme za Kiarabu wiki ya kwanza ya mwezi Machi, kwa mujibu wa mamlaka.
  Sudan imesitisha utoaji wa visa kwa nchi 8 ikiwemo Italia na nchi jirani ya Misri kwa hofu ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
  Nchini Misri, usafiri wa basi pia umesitishwa.
  Misri ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kuthibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya corona pamoja na vifo viwili vya ugonjwa huo huku visa 80 vikiripotiwa.
  Aidha, kisa cha kwanza cha virusi vya corona kimethibitishwa nchini Kenya. Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kwamba mtu mwenye maambikizi ya virusi vya Corona alithibitishwa kuwa ana maambukizi hayo Alhamisi usiku.
  Nchini Ethiopia mamlaka za nchi hiyo pia imetangaza kisa cha kwanza cha maambukizi ya coronavirus.
  Mgonjwa wa Ethiopia ni raia wa Japani.

Post a Comment

0 Comments