Coronavirus: Viwanja vya ndege Marekani vyashuhudia wimbi la misururu mirefu ya ukaguzi

Ghasia zimeshuhudiwa katika viwanja vya ndege vya Marekani wakati ambapo hatua mpya za ukaguzi kwasababu ya virusi cha Corona zinaanza kutekelezwa dhidi ya watu wanaorejea nchini humo kutoka Ulaya.
Kumekuwa na foleni ndefu huku wasafiri wakisubiri kwa saa kadhaa kukaguliwa kabla ya kupita kwenye ofisi za forodha.
Awali, makamu rais wa Marekani Mike Pence alisema kuwa Uingereza na Ireland Jumanne zitaongezwa kwenye orodha ya nchi zilizopigwa marufuku kuingia nchini humo pamoja nchi zingine za Ulaya zilizotambuliwa.
Marekani ina visa zaidi ya 2,700 vya corona huku vifo 54 vikiwa tayari vimethibitishwa.
Wachambuzi wanasema kwamba kwa sasa hali ya taharuki imetanda nchini Marekani huku kukiwa na hofu ya huduma za hospitali kutoweza kufikia wote wenye hitaji la haraka pamoja na huduma kwa watoto wakati ambapo mamilioni ya wanafunzi wanarejea nyumbani.
Matukio mengine:
  • Shirika la ndege la Marekani limesema kwamba linapanga kusitisha huduma zake za safari za kimataifa kwa asilimia 75 hadi May 6.
  • Ganama wa Oklahoma Kevin Stitt amekuwa na wakati mgumu katika mtandao wa Twitter, baada ya kuonekana kwa picha zinazomuoesha yeye na familia yake wakiwa kwenye mgahawa uliokuwa umejaa watu.
  • Wapiga kura nchini Ufaransa watashiriki uchaguzi wa mitaa ambao umepangiwa kufanyika licha ya mlipuko wa ugonjwa wa corona
  • Australia imetangaza kwamba wasafiri wote wanaowasilinchini humo kuanzia usiku wa manane saa za eneo Jumamosi, ni lazima wajitenge binafsi kwa wiki mbili.
  • Waziri wa Afya wa Uingereza Matt Hancock amesema kuna mipango katika wiki zijazo ya kujitenga binafsi kwa yeyote mwenye umri wa miaka 70 na zaidi
Nini kimekuwa kinachoendelea katika viwanja vya ndege Marekani?
Katika viwanja vya ndege vya At Chicago O'Hare na Dallas DFW, kumekuwa na foleni ndefu za wasafiri wanaorejea nchini humo kutoka Ulaya wakisubiri kukaguliwa kama sehemu ya hatua za kukabiliana na virusi vya Corona.
Utawala wa Marekani umeweka marufuku kwa raia ambao si wa Marekani kutoka mataifa 26 ya Ulaya katika eneo la ukanda huru la Schengen na marufuku hiyo inatarajiwa kujumuisha Uingereza na Ireland kuanzia Jumanne.
Raia wa Marekani wanaruhusiwa kurejea nchini humo lakini lazima wafanyiwe ukaguzi.
Gavana wa jimbo la Illinois JB Pritzker amesema kuwa foleni hizo ndefu katika uwanja wa ndege wa O'Hare ni jambo lisilokubalika.

Post a Comment

0 Comments