Coronavirus:Wauguzi wa wagonjwa waliombukizwa virusi vya corona Kenya waanza mgomo baridi

TOP STORIES
Wauguzi wanaofanya kazi katika wodi iliyotengwa kwa watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Kenya wameanza mgomo baridi kulalamikia kile wanachodai kuwa ukosefu wa vifaa vya kujikinga na mafunzo ya kutosha.
Hospitali ya Mbagathi katika mji mkuu wa Nairobi, ni moja ya hospitali zilizo na wodi ya kutibu wagonjwa waliombukizwa virusi hivyo hatari.
Katibu mkuu wa muunganowa wauguzi nchini Kenya,Seth Panyako ameiambia BBC kwamba wauguzi watarejea kazini ikiwa watapewa mavazi maalum na mafunzo ya jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa.
"Wahudumu wa afya wako katika hatari ya kupata maambukizi katika mazingira yao ya kazi," alisema Bw. Panyako.
"Bila ya kuwa na vifaa maalum,wanatarajiwa kujilinda vipiwakiwa kazini na wanaporejea nyumbani kutangamana na familia zao?"
Hospitali ya ya Mbagathi inawazuilia watu 22 ambao walitangamana na mgonjwa wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya corona.
Watu wengine wawili walioambukizwa virusi hivyo wamepelekwa katika hospitali ya ya kitaifa wa Kenyatta - ambako mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa kuambukizwa anapewa matibabu.
Wataalam wa afya ya umma wamekuwa wakitoa ushauri ili kujaribu kuzuia maambukizi ya virusi hivi.
Kenya kwa sasa inakabiliwa na kibarua kigumu cha kuwatafuta wale waliotangamana na watu watatu waliothibitishwa kuambukizwa vitrusi vya corona.
Akizungumza na BBC Msemaji wa serikali Bw. Cyrus Oguna amesema serikali itatoa maelezo zaidi shughuli hiyo imefika wapi.
''Kwa kweli kuna changamoto zipo na tunakubali mazingira yetu utaratibu wa kuweza kujua mtu anaishi wapi'' alisema Bw. Oguna.
Hata hivyo ametoa wito kwa watu ambao huenda wa wametangamana na wagonjwa watatu walioambukizwa virusi hivyo kufika katika kituo cha afya kilicho karibu nao.

Je ni lazima kuwa na kemikali za kuua viini yaani sanitizers?

Serikali ya kenya imefahamisha raia kwamba hakuna haja ya kuwa na hofu licha ya kuthibitishwa kwa kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona.
Kulingana na mwandishi wa BBC kitengo cha Afya Rhoda Odhiambo, katika mitandao ya kijamii kuna mengi ambayo yanapotosha kuhusu ugonjwa wa Corona.
Kwa sasa ni kwamba hakuna haja ya kununua kwa wingi kemikali za kuosha mikono zinazoua viini kwa haraka au hata kununua bidhaa kwa wingi kwasababu ya hofu ya ugonjwa huu.
An empty hand sanitiser shelf in Superdrug in London

Maagizo yaliotolewa na wizara ya afya Kenya

Kunawa mikono mara kwa mara.
 • Kutokaribiana sana na mtu mwingine ambaye anakohoa ama kupiga chafya - simama umbali wa mita moja
 • Watu wanaokohoa ama kupiga chafya wasalie majumbani mwao ama kutojichanganya na makundi ya watu
 • Hakikisha kwamba unaziba pua na mdomo unapokohoa kwa kutumia kitambaa ama tishu.
 • Mtu anayehisi joto ama tatizo la kupumua ametakiwa kusalia nyumbani.
 • Tumepiga marufuku mikutano ya aina yote ikiwemo ile ya umma kama vile ya kidini, michezo, na wanaotaka kwenda makanisani na msikitini watalazimika kuosha mikono na sabuni kabla ya kuingia katika sehemu hizo.
 • Michezo yote inayohusisha shule imepigwa marufuku lakini shule zote zitasalia wazi kwa wakati huu.
 • Wachukuzi wa umma wametakiwa kuhakikisha kuwa abiria wanaosha mikono yao kabla ya kuingia katika magari hayo.
 • Amewaonya Wakenya kutosambaza habari za uongo kuhusu virusi hivyo katika mitandao ya kijamii ambazo zinaweza kusababisha hofu.
 • Wakenya wamewekewa zuio la kutoka nje ya nchi isipokuwa wale wenye umuhimu mkubwa wa kusafiri na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuelekea katika mataifa yenye visa vingi vya ugonjwa huo.
 • Serikali imesema kwamba itatoa maelezo kuhusu ugonjwa huo kila siku.
 • Waziri huyo amesema kwamba Kenya inaelekea katika wakati ambapo sekta za kibinafsi na zile za kibiashara zitalazimika kuisaidia serikali na raia katika kuchukua jukumu la kukabialana na janga hili.
 •  Kasi ya kusambaa kwa virusi 16 Machi 2020
Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.

Post a Comment

0 Comments