INASISIMUA! Kifo Usiku wa Honeymoon


*DEATH ON HONEYMOON’S NIGHT*
WAKIWA ndiyo kwanza wametoka ukumbini kufunga ndoa, Patrick Mshana na Vera Mosha wanaingia katika hoteli ya kifahari, Shirimatunda Lounge kwa ajili ya fungate lao la kwanza.

Walipanga kukaa hapo kwa siku nne kabla ya kwenda Zanzibar kumalizia fungate lao. Wakiwa kitandani, wakifurahia tendo la ndoa la kwanza ndani ya ndoa yao, hawakujua chini ya uvungu, kulikuwa na Filipo aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Vera.
Filipo alitumia mbinu za kijasusi kuingia ndani ya chumba hicho na kujichimbia uvunguni akisubiri kutekeleza kisasi cha kifo.

Filipo aliyekuwa askari mpelelezi, hakukubali kuachwa na Vera ghafla kwa sababu ya Patrick, kijana msomi aliyekuwa MKurugenzi wa Mamlaka ya Kodi na Uchumi, Mkoa wa Kilimanjaro.
Asubuhi yake, Insp. Filipo anamuua Vera kwa kummiminia risasi. Ni muda mfupi baada ya Patrick kuondoka kidogo, kuelekea nyumbani kuchukua kompyuta kwa ajili ya kazi za ofisini.

Hakujua nyuma kulifanyika mauaji hayo. Haraka Insp. Filipo anaondoka, ambapo anafuatwa na rafiki yake aitwaye James ambaye wanatokomea zao, Asteria Hotel iliyopo Machame – Nkwarungo kujificha. Huko wanajipongeza kwa kunywa pombe na kuchoma nyama.

Harusi inageuka msiba. Faili la Kesi linatua mikononi mwa Insp. Shembiu ambaye anahangaika kumsaka muuaji. Hakujua kuwa muuaji ni mpelelezi mwenzake, Insp. Filipo.
Insp. Shembiu anahojiana na meneja wa hoteli hiyo, hakuna alichofanikiwa. Hata alipomuhoji Patrick, bado hakupata mwanga. Anahisi kuchanganyikiwa!

Akajiambia: “Lakini lazima ampate muuaji. Lazima apatikane. Nitampata tu.”
Je, nini kitatokea? , Usikose sehemu inayo fuata imeandaliwana NADHIRI.A.RASHIDI

Post a Comment

0 Comments