Jokate atajwa kwenye orodha ya wanawake 50 Afrika wenye mchango kwa jamii

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo  ametajwa kwenye orodha ya Wanawake 50 Afrika wenye mchango kwenye jamii yao na Shirika la ‘Donors for Africa’ la Nigeria.

 Chidi Koldsweat ni Boss wa Shirika hilo amesema Wanawake waliotajwa ni wale ambao wameleta mabadiliko chanya kwa jamii kupitia kazi zao kwenye Mashirika ya Kimataifa, Tasisi za Serikali na binafsi, Siasa , Sekta ya Habari n.k

"Nimefurahi kutajwa imenipa nguvu kuendelea kupambana, Wanawake wenzangu wajitambue, tambua Mungu amekupa nini, itakusaidia kuweka mipango ya kuleta maendeleo sio kwako tu hadi kwa jamii"- Jokate

Post a Comment

0 Comments