MICHEZO Mambo manne yanayoweza kuamuliwa EPL, kama corona itaendelea

Hadi sasa virusi vya Covid 19 vinavyosababisha homa kali ya mapafu ya corona vimethibitika kuenea sehemu mbalimbali duniani na kusitisha kazi na baadhi ya shughuli.
Kwa upande wa soka Ligi tano kunwa ulaya zimetangaza kuahirisha michezo yao hadi April 3 ndio watatangaza maamuzi tofauti kulingana na hali ya maambukizi nchini humo yatakavyokuwa.
Ligi Kuu ya Hispania LaLiga, Serie A, Ligue 1, Bundesliga pamoja na Ligi Kuu England zimesimama huku kukiwa na ubashiri kuwa kama maambukizi yataendelea zaidi EPL wanaweza kuchukua hatua moja kati ya nne zifuatazo.
1- Kuna uwezekano Ligi ikaendelea ila mechi zikachezwa bila mashabiki uwanjani.
2- Kuahirisha tena Ligi hadi watakapotangaza tena tarehe.
3- Kufuta msimu na matokeo yaliyopo yaendelee kuwa kama yalivyo katika msimamo, Bingwa awe Liverpool.
4- Kufuta msimu mzima wa 2019/20 na kusubiri kuanza kwa msimu 2020/21 pasipo kuwa na Bingwa wala timu iliyoshuka daraja ya 2019/20.

Post a Comment

0 Comments