MICHEZO Simba SC yatangaza kumkosa Erasto Nyoni

Beki wa Simba SC Erasto Nyoni kwa mujibu wa ukurasa rasmi wa club hiyo umetoa taarifa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.
Erasto atakuwa nje ya uwanja kwa sababu ya kuuguza jeraha lake la kifundo cha mguu alichoumia wakati wa mchezo wa Simba na Yanga ambao uliisha Simba ikipoteza 1-0.
Hata hivyo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Etienne Ndairagije amemuita katika kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na fainali za CHAN na mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021.

Post a Comment

0 Comments