Mufti Mkuu wa Tanzania “Ni haramu mwenye Corona kwenda Msikitini

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir leo March 18,2020 amesema kwa Muislamu atakayepata virusi vya corona ni haramu kwake kuhudhuria swala ya Ijumaa na swala za Jamaa Msikitini kwani kufanya hivyo ni kuusambaza ugonjwa huo kitu ambacho ni haramu.
Mufti Zubeir ameagiza pia kufungwa kwa Madrasa zote pia amewataka Waislamu kutii amri za karantini pale itakapotolewa.

Post a Comment

0 Comments