Mwingine Akutwa na Corona Congo DR

KISA cha pili cha maambukizi ya ugonjwa wa Corona-virus kimethibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mtu huyo anadaiwa kuwa raia wa Cameroon aliyewasili nchini humo kutoka Ufaransa kulingana na mwandishi wa BBC mjini Kinshasa.

Kwa sasa amelazwa hospitalini kwa matibabu. Wizara ya afya nchini humo imetoa wito kwa raia kuzingatia usafi wakati wowote. Mgonjwa huyo ana umri wa miaka 46 ambaye anaishi nchini humo na familia yake.

Alirudi nchini humo kutoka Ufaransa mwezi Mei 8 na hakuonyesha dalili za virusi hivyo. Mamlaka nchini humo inasema kwamba kufikia sasa imewatambua watu 117 waliogusana na wagonjwa wawili wa virusi hivyo.

Habari hiyo inajiri siku moja baada ya madaktari nchini humo kuamua kurudi kazini wakisitisha mgomo wa miezi miwili. Mwandishi wa BBC anasema kwamba muungano wa madaktari ulikubaliana na serikali kuimarisha mazingira yao ya kazi.

Waziri wa afya, Eteni Longondo, ametoa wito wa utulivu na kuzingatia usafi kwa kuosha mikono yao mara kwa mara. Congo ni nchi ya 11 ya Afrika kuthibitisha maambukizi ya ugonjwa hatari wa Covid-19 ulioanzia China  na umewua zaidi ya watu 3 800.

Congo kwa sasa imeimarisha uchunguzi katika viwanja vyake vinne vikuu vya ndege kwa kuwakagua kwa makini wasafiri walio na viwango vya juu vya joto, hatua ambayo imekuwa ikichukuliwa kama sehemu ya kupambana na maambukizi ya virusi hatari vya Ebola.

Post a Comment

0 Comments