Nahodha wa Samatta apigwa faini licha ya kupata ajali ya gari, kisa Corona


Naohdha wa klabu ya Aston Villa anayochezea Mtanzania Mbwana Ally Samatta amelazimika kupigwa faini na kilabu yake licha ya kuomba radhi kwa kukaidi agizo la serikali la kukaa ndani kipindi hiki cha janga la virusi vya #corona.
 Klabu yake ya Aston Villa, Imethibitisha kuwa, itamchukulia hatua za kinidhamu na kumlipishwa faini ya £150,000 ambayo ni sawa na Tsh milioni 379,828,822.20 ambayo itatolewa kama msaada katika Hospitali ya kijamii ya ya Chuo Kikuu cha Birmingham.
Mbali na faini hiyo Kiungo huyo pia wa klabu ya Aston Villa na timu ya taifa ya Uingereza alinusurika katika ajali ambapo aligongesha gari lake la kifahari Range Rover yenye thamani ya £80,000 ambayo ni sawa na Tsh milioni 202575371.84 kwenye gari mbili ambazo zilikuwa zimepaki ambazo ni silver C-Class Mercedes yenye thamni ya £30,000 , na blue Mercedes yenye thamni ya £20,000.Zote ameshalipa.
Kupitia kamera za CCTV majirani pia waliongea na kusema kuwa “Jack alionekana ni mtu ambaye alikuwa amepanga kutoka kwani alionekana akiwaaga baadhi ya watu aliokuwa nao kwa kugongesha mabega yao”
Jirani mwingine alisema kuwa “Katika nyumba ya Jack kulionekana kama kuwakuwa na party (Sherehe ) kwani kulikuwa na kelele sana lakini ilipofika majira ya 8:Am kelele zilikata na baada ya muda ndio tukapata habari z atukio hili”
Kutokana na baadhi ya mashuhuda inaonyesha kuwa Jack huenda alilewa kutokana na party alikuwa akiifanya nyumbani kwake. Licha ya hivyo Jack alionekana akiwa amevaa viatu tofauti tofauti moja cheupe na kingine cheusi.
Kabla ya tukio hilo Jack alipost kupitia ukurasa wake wa Twitter akiwahimiza watu kukaa ndani na kutokutoka lakini baada ya muda yeye alitoka na baada ya muda aliomba msamaha.

Post a Comment

0 Comments