Namungo Fc Yaibana Mbavu Yanga Leo Majaliwa, Wagawana Pointi Mojamoja


NAMUNGO FC leo imeibana mbavu Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa kwa kulazimsiha sare ya kufungana bao 1-1.

Yanga ilianza kuinyoosha Namungo FC dk ya sita kupitia kwa Tariq Seif liliwapeleka Namungo vyumba vya mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Namungo FC walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Bigirimana Blaise dakika ya 62.

Sare hiyo inaifanya Namungo kufikisha pointi 50 ikiwa nafasi ya nne huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 51.

Post a Comment

0 Comments