Premier League waja nampango mkakati dhidi ya Corona, mechi 92 zilizobaki lazima zipigwe

Ligi kuu nchini England maarufu kama Premier League imekuja na mpango mkakati katika kuhakikisha msimu unamalizika bila kusimamishwa.

Kutokana na kuibuka kwa janga la ugonjwa wa Corona ligi nyingi duniani zimesimama ili kuepuka kuenea zaidi kwa virusi hivyo hali iliyofanya Premier League kuja nampango wa kuhakikisha jumla ya mechi zake 92 zilizo salia zinachezwa, hivyo wapo tayari michezo hiyo kupigwa bila mashabiki na badala yake kurushwa mubashara kupitia Luninga.
Kwa mujibu wa The Sun, huwenda michezo hiyo ikapigwa kwenye viwanja viwili au vitatu ambavyo vitakuwa havina mashabiki.

Post a Comment

0 Comments