Rais wa Real Madrid afaraki kwa Virusi vya Corona

Rais wazamani wa klabu ya Real Madrid, Lorenzo Sanz amefariki dunia akiwa hospitali kutibiwa Virusi vya Corona.
Sanz mwenye umri wa miaka  76, amekuwa rais ndani ya Bernabeu kuanzia mwaka 1995 hadi 2000 huku katika kipindi chake cha uongozi akifanikiwa kutwaa Champions League mara mbili.
Ujumbe aliyoandika mtoto wake, Lorenzo Sanz Duran kupitia akaunti yake ya kijamii ya twitter “Baba yangu amefariki dunia”
Sanz akiwa katika madaraka aliweza kumsajili, Roberto Carlos, Clarence Seedorf na Davor Suker ndani ya Real Madrid
Mwaka 2000 alipoteza katika uchaguzi na nafasi yake kuchukuliwa na Florentino Perez.

Post a Comment

0 Comments