WHO yatilia mashaka vipimo vya Corona Afrika

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Ghebreyesus amesema idadi ya Wagonjwa wa virusi vya Corona inayoripotiwa Afrika huenda siyo sahihi kwa kuwa vipimo siyo thabiti.
Kauli hiyo ya Tedros inakuja muda mchache baada ya Burkina Faso kutangaza kifo cha kwanza kutokana Corona nchini humo na kuuangana na nchi za Misri,Morocco, Algeria, Senegal, Tunisia.
Taarifa nchini Burkina Faso zinasema aliyefariki ni Mwanamke (62) aliyekuwa anaugua pia Kisukari lakini taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai aliyefariki ni Rose Marie Compaore aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Bunge.

Post a Comment

0 Comments