Xavi kurejea Barcelona, ataja listi ya nyota anaowataka, lipo jina la mchezaji ghali duniani

Legend wa Barcelona, Xavier Hernandez amefunguka kuwa yupo tayari kurudi ndani ya miamba hiyo ya soka ya Hispania kama Kocha Mkuu lakini ametaja masharti yake kwa klabu hiyo.
Kiungo huyo wazamani wa Nou Camp alipewa nafasi ya kurithi mikoba ya Ernesto Valverde hapo mwaka jana lakini hatimaye alikataa fursa hiyo.
Lakini baadae Barcelona ilihamia kwa Quique Setien na kukiongoza kikosi hiko na kufanikiwa kuleta ushindani mkubwa dhidi ya Real Madrid ndani ya La Liga.
Baada ya mchezo wa mpira wa miguu kusimama kwa muda kufuatia mapambano dhidi ya virusi vya Corona habari za Xavi kurejea Barcelona akitoka kuifundisha Al Sadd ya Qatar, zimeanza kushika kasi upya.
Xavi ameliambia gazeti la Hispania la La Vanguardi kuwa “Naweka wazi kuwa nataka kurudi Barcelona, nimevutiwa sana.”
“Pengine miaka iliyopita ningeliweza kujipa heshima mwenyewe, lakini kwa sasa nimejiona mwenyewe ninavyofundisha, ninaweza kabisa kuwapatia kitu wachezaji.”
“Ningelipenda kufanya kazi pamoja na watu ambao nina imani nao, watu ambao waaminifu na watakao kuwa sahihi.”
Kwa upande wa usajili Xavi amewaweka wazi baadhi ya nyota ambao angependa kuwa nao “Ningependa kusajali winga kama Neymar, Jadon Sancho, Serge Gnabry. Barcelona tayari inawachezaji wa kucheza kati lakini mapungufu yaliopo ni upande wa winga kama vile ilivyo Bayern. Haitaji sura mpya nyi bali wachache tu.”
Hata hivyo amehofia mambo ya kimahusiano huwenda yakaleta uzito katika kumsajili Neymar kutokana na namna alivyoondoka ndani ya Barcelona.
Barcelona inamkataba na Quique Setien mpaka 2022, lakini Xavi amefungua milango kwa klabu yake kama watahitaji kuhuduma yake ya kuifundisha miamba hiyo ya soka ya La Liga.

Post a Comment

0 Comments