Kupitia akaunti yao ya kijamii ya Instagram Yanga imeandika ”Daima furaha na Amani ya Wanayanga huletwa na wenye upendo wa dhati na timu yao. Tuendelee kuijenga Yanga SC.”
Siku za hivi karibu timu hiyo ya Wananchi imekubwa na jinamizi la kutokuelewana ndani ya uongozi hadi kupelekea wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu kama vile Said Rupia na Frank Kamugisha huku wengine wakijiuzulu yote yakiibuka baada ya kuenea kwa taarifa za mdhamini wa klabu hiyo GSM kutangaza kupunguza majukumu yake kwa Wanajangwani hao
0 Comments