Zlatan aanzisha mfuko wa kusaidia waathirika wa Corona Italia, Kauli yake “Kama Corona haijaenda kwa Zlatan basi Zlatan ataifuata Corona” Zlatan aanzisha mfuko wa kusaidia waathirika wa Corona Italia, Kauli yake "Kama Corona haijaenda kwa Zlatan basi Zlatan ataifuata Corona

Mshambuliaji wa klabu ya AC Milan ya Italia na aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic siku ya jana amezindua rasmi kampeni ya kufadhili na kusaidia namna ya kupambana na janga la Virusi vya Corona.
Ibrahimovic amezindua mfuko wa kusaidia kupambana na Corona Virus na ametoa wito kwa wachezaji wenzake kusaidia mapambano dhidi ya “kupigana na virusi hivi”.
Mshambuliaji huyo wa AC Milan anacheza Italia, nchi ambayo imeathiriwa zaidi na janga hili baada ya China.
“Taifa la Italia daima imekuwa likinisaidia sana, Lakini katika wakati huu mgumu, nataka kurudisha kwa jamii zaidi kwa nchi hii ambayo ninaipenda mno. Niliamua, pamoja na watu wanaofanya kazi na mimi, kuunda mfuko wa fedha kwa ajili ya hospitali kutumia ukubwa wangu kueneza ujumbe huu kote”
Hili ni tatizo kubwa na la ukweli kabisa tunahitaji msaada zaidi wa vitendo sio tu kurekodi video.
Ninategemea ukarimu wa wenzangu, yaani wachezaji wenzangu wanaotaka kutoa mchango mdogo au mkubwa kulingana na uwezo wao, ili kukabiliana na virusi hivi”
Kwa pamoja tunaweza kusaidia hospitali na madaktari na wauguzi ambao kwa hiari wanafanya kazi kila siku kuokoa maisha yetu.
Na kumbuka: ikiwa virusi haviendi kwa Zlatan, Zlatan ataenda na kuvifuata virusi!

Post a Comment

0 Comments