Aliwahi Kunifumania, Nami Nimemfumania Leo..Vipi Wadau Nimpige Chini?

Nikiwa niko kwenye Karantini la Maskani, ghafla jamaa yangu anakuja mbio mbio.

" Brother wanawake ni mbwa kabisa, nimetoka kumfumania shemeji yako na Bwn.Lambalamba Kachupi saiv! Japo sijakuta wamelala, lkn walikuwa wanapeana chakula cha ndege (sijui ndo lile busu la kifaransa) pale kwa Shemeji yako". Akaendelea "Imeniuma Sana kaka. Mi nampiga chini, Siataki ushauri, nakushirikisha tu maamzi yangu". Akaondoka.


IKO HIVI.
Huyu rafiki yangu, ni ukweli wa kweli kwamba hajatulia kabisa, kuna wakati kama binadamu huwa namhurumia huyu shemeji yangu, kwa maana alisha mfumania mara kibao sema anasamehe.

Ikumbukwe kuwa ni wachumba ambao wamesha tambulishana kwa wazazi na marafiki.

Jamaa hajawahi kuwa na wasiwasi na mchumba wake, anampenda Sana mengine ni tamaa tu za ujana.

Leo ni mara ya kwanza anamfuma na kutoa maamzi ya kuachana. Binafsi namuona huyu dada Kama mtu mmoja muelewa na muungwana Sana. Sihitaji rafiki yangu aachane nae. Nahitaji kuona wakioana.

Shemeji amenitumia meseji kwamba anampenda Sana jamaa yangu, sema Kuna wakati kama binadamu anaumia Sana.

Kaapa kutorudia na kwamba, Bwn Lambalamba Kachupi hajagusa Water table yake.

Kwa nafasi yako ungeli-handle vipi hili jaribu?

Nawasilisha!

Post a Comment

0 Comments