Chad: Mwandishi wa habari Martin Inoua Doulguet aachiliwa kwa dhamana

Mahakama ya Rufaa ya Ndjamena imechukuwa uamuzi wa kumuachilia kwa dhamana mwandishi wa habari Martin Inoua Doulguet, kwa mujibu wa wakili wake
Martin Inoua Doulguet, ambaye alikamatwa kwa makosa "kashfa dhidi ya viongozi" mwezi Agosti 2019, katika mahakama ya mwanzo, alihukumiwa kifungo cha miaka 3, huku akitakiwa kulipa fidia ya Euro 15,000 na faini ya Euro 3,000 kwa makosa ya "kushirikiana na kundi la maharamia wa mtandao" mara ya kwanza mwezi mmoja baadaye.
Shirika la Wanahabari wasio na Mipaka, RSF, na mashirika mengi ya haki za binadamu nchini Chad yalilaani mara kadhaa hukumu hiyo na mazingira mbaya ya kuzuiliwa kwake.
Chad imeendelea kunyooshewa kidole cha lawama na mashirika ya haki za binadamu kwa kuvunja haki za waandishi wa habari, na kukiuka mikataba mbalimbali ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Post a Comment

0 Comments