China yaiomba Marekani kutimiza wajibu wake kwa WHO

China imeiomba Marekani hii leo kutimiza wajibu wake kwa shirika la afya ulimwenguni, WHO baada ya Rais Donald Trump kusimamisha ufadhili kwa shirika hilo akilituhumu kushindwa kulishughulikia ipasavyo janga la virusi vya corona.

Waziri wa mambo ya kigeni wa China Zhao Lijian amewaambia waandishi wa habari alipozungumzia hali ya virusi hivyo ambavyo vimewaambukiza takriban watu milioni 2 kote ulimwenguni kwamba uamuzi huo wa Marekani huenda ukaathiri mataifa yote ulimwenguni.

Mjini Berlin, waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Heiko Maas amezungumzia uamuzi huo wa Marekani akisema uimarishwaji wa shirika hilo ni moja ya uwekezaji muhimu. Maas ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba lawama hazitasaidia kwa kuwa virusi hivyo havina mipaka.

Post a Comment

0 Comments