CORONA: Biashara duniani zimepungua kwa asilimia 13

Ripoti mpya kuhusu Takwimu na Makadirio ya Biashara ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) imesema, biashara duniani zinakadiriwa kupungua kwa asilimia 13 hadi asilimia 32 kwa mwaka 2020 ikiwa ni athari za mlipuko wa COVID 19.
Kupungua huko kunaweza kuwa kubaya kuliko kuporomoka kwa biashara kulikosababishwa na msukosuko wa fedha wa Kimataifa wa mwaka 2008, na kwamba Amerika Kaskazini na Asia zitaathirika zaidi.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, biashara duniani zinatarajiwa kufufuka kwa asilimia 21 hadi 24 mwaka 2021, endapo mlipuko wa virusi vya Corona utadhibitiwa.


Post a Comment

0 Comments