DRC: Washirika wa Vital Kamerhe wajaribu kukutana na utawala

Vital Kamerhe, Mkurugenzi wa ofisi ya rais na mshirika wa rais Felix Tshisekedi, bado anazuiliwa katika gereza kuu la Makala jijini Kinshasa, huku baadhi ya makada wa chama cha UNC wakijaribu kukutana na utawala kuomba kiongozi wao aachiliwe huru.
MATANGAZO YA KIBIASHARA
Zoezi la kuwasikilizi yeye na wenzake wanaoshtumiwa ufisadi katika mpango wa dharura wa rais Félix Tshisekedi limemalizika, lakini bado anaendelea kuzuiliwa.
Kwa upande wake, Bw Kamerhe anasema bado hajakata tamaa. Kulingana na washirika wake wa karibu, anaendelea kuamini makubaliano yaliyopo kati yake na Félix Tshisekedi.
Makada kadhaa wa chama cha UNC hawafurahi wito uliotolewa na Vital Kamerhe wa kuwataka wawe watulivu na kutothubutu kuzungumzia chochote kwenye vypmbo vya habari.
Bado hawaamini kuwa Félix Tshisekedi alikubali mkurugenzi katika ofisi yake "adhalilishwe".
Kudhalilishwa ni neno ambalo mara nyingi hurejelewa katika taarifa zinazotolewa na chama cha UNC.
Upande wa ikulu ya rais, vyanzo kadhaa vinbaini kwamba Félix Tshisekedi anataka mahakama ifanye kazi yake na sheria ifuate mkondo wake, wahusika waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande mwingine mkewe Vital Kamerhen Hamida Shatur anaendelea kukutana kwa mazungumzo na mkewe rais Tshisekedi, Denise Nyakeru Tshisekedi, huku akiamini kwamba mumewe ataachiliwa huru

Post a Comment

0 Comments