GSM Wasaini Mkataba Mwingine Mpya Yanga

YANGA kumenoga! Hivyo ndivyo utakavyoweza kusema baada ya timu hiyo kuingia makubaliano mengine na mdhamini wake Kampuni ya GSM ya kusaini mkataba mpya mwingine kwa ajili ya kutumia nembo ya klabu hiyo kutengeneza na kuuza vifaa mbalimbali.

GSM wameingia makubaliano hayo ikiwa ni siku chache tangu watangaze kurejea Yanga baada ya awali kuwepo taarifa za kujitoa kwenye sehemu ya udhamini wa klabu hiyo baada ya kutokea mtafaruku kati ya baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji ya timu hiyo na mdhamini huyo.

Kampuni hiyo imeonekana kurejea kwa kasi Yanga baada ya kutangaza kufanya usajili wa mchezaji yeyote atakayependekezwa katika usajili wa msimu ujao kwa gharama yoyote lengo ni kuhakikisha wanauchukua ubingwa wa ligi msimu ujao.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injia Hersi Said, mka-taba huo unata-rajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2021 baada ya kusaini-shana mikataba na viongozi wa klabu hiyo.

Hersi alisema kuwa mkataba huo walioingia wa kutengeneza bidhaa za klabu (Club Merchandise) zitakazokuwa na chapa ya Yanga SC zitakazouzwa na mashabiki wa timu hiyo, utaipa fursa Kampuni ya GSM kutumia chapa ya Yanga kutengeneza bidhaa nyingine tofauti na jezi.

Injinia huyo alizitaja bidhaa hizo kuwa traki suti, t-shirts, vikombe, saa, viatu (raba na sandozi), bracelets na nyingine nyingi ambazo watazingeneza ambazo zitaanza kuuzwa mwaka 2021.“Hii ni moja ya njia ambayo itaongeza mapato kwenye klabu yetu ya Yanga kutokana na mauzo yatokanayo na bidhaa hizo zitakazo zalishwa na Kampuni ya GSM.

“Tunaamini hii ni njia sahihi kwa Yanga kujiingizia kipato, kama mnavyofahamu kuendesha timu kubwa tena kama ya Yanga ni gharama, hivyo ni lazima vyanzo vya mapato viwe vingi.

“Hivyo, basi sisi GSM tumeona tuingie makubaliano mengine mazuri kwa manufaa ya klabu yetu pendwa ya Yanga kwa kusaini mkataba mwingine mnono wa kuuza bidhaa mbalimbali kama vile kofia, t-shirts, vikombe na vingine vingi watakavyovitumia mashabiki wetu na mkataba huo utaanza rasmi 2021,” alisema Hersi.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alizungumzia hilo kwa kusema: “Kama tulivyoahidi katika kipindi chetu cha kampeni wakati wa uchaguzi ni kuhakikisha Yanga tunawaweka karibu na wanachama na kingine kuongeza vyanzo vya kupata fedha ikiwemo kuongeza udhamini.

“Hivyo, hicho ndiyo tunachokifanya hivi sasa, tayari tumefikia makubaliano mazuri na GSM kusaini mkataba mpya ambao tofauti na jezi wakitumia nembo ya klabu kutengeneza bidhaa nyingine kwenda kwa mashabiki.

Post a Comment

0 Comments