HABARI ZA MASTAA Burna BOY kuja na album mpya ‘Twice as Tall’ mwezi July mwaka huu

Ni Mkali kutokea Nigeria, Burna Boy ambae baada ya The African Giant kufanya vizuri sokoni sasa ameujuza umma kupitia mtandao wake wa twitter kuwa anatarajia kuileta album yake nyingine aliyoipa jina la Twice as Tall.
Staa huyo aliweka wazi taarifa hizo baada ya shabiki kumuuliza swali na kupelekea kuitaja rasmi mwezi atakaoachia album hiyo mpya.
Burna Boy aliandika ‘Najisikia vibaya sana mama yangu kwenye muziki, Angelique Kidjo alinieleza  kila kitu ninachotakiwa kuelewa kuhusu tuzo za Grammys na sasa twice as Tall ndio jina la album yangu inayofuata nitakayoiachia mwezi July’- Burna Boy

Post a Comment

0 Comments