Hatua mpya zatangazwa Uturuki kukabiliana na virusi vya corona

Rais wa Uturuki ametangaza hatua mpya  za kuzingatiwa katika juhudi za kukabiliana na kupambana na virusi vya corona nchini Uturuki.

Hatua hizo zimetangazwa  usiku wa Ijumaa katika mkutano na wanahabari.

Rais Erdoğan amesema kuwa hatua hizo  zimechukuliwa  baada ya mkutano wa  jopo la wanasayansi wa Uturuki na wataalamu wa afya.

Hatua hizo zimeanza kuheshimishwa  kuanzia wakati huo aliotangaza kupitia runinga Ijumaa.

Hatua zilizochukuliwa ni :

- Marufuku kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka  20 kutoka nje.
-  Marufuku  ya kusafiri , kuingia na kutoka katika miji 31.
- Agizo la kuvaa barakoa .

Vile vile imetangazwa kuwa  adhabu kali itatolewa kwa yeyote atakae kiuka maagizo hayo.

Rais Erdoğan amesema kuwa  hatua hizo hazichukuliwa kwa kuwakanzamiza raia bali kujali afya na usalama wa taifa zima, huku akimalizia kwa kusema kuwa kurejea katika hali ya kawaidi kutatokana na  nyendo zetu na kuzingatia  maagizo kutoka serikalini.

Post a Comment

0 Comments