Hivi we Mwanaume Mkeo ‘Akiliwa’ nje Kinachokuumiza ni Nini Hasa? Mbona Nyie Mnawala Wake wa Wenzenu?

Hii dunia haiko fair..!

Kuna wanaoamini mke wa mtu sumu, hapo hapo kuna imani kuwa wake za watu ni ‘rahisi’ kuwapata, hawana longolongo.

Na hizo kauli zote ni za wanaume, lakini inapotokea ukahisi au ukajua mkeo analiwa ni lazima roho ikuume.

Mkeo ameliwa kwa ridhaa yake, huenda nawe umewahi kula mke wa mwenzio, kinachokutoa roho ni kipi.?

Je ni kudharaulika, kwamba kanionaje, au niaje.?

Hebu tujadili bila hasira, lazima kila mtu anarespondi kwa namna yake. Kwa wale ambao yashawakuta watupe uzoefu, na wale ambao bado [japo hatuombei] ikitokea watafanyaje.?

Post a Comment

0 Comments