Kagere: Wananiita mzee ila ninawafunga

MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa wanaomuita mzee hawashangai kwani wanampa nguvu ya kupambana kufunga akiwa uwanjani.

Kagere kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa Machi 17 kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona alikuwa na mabao 19 akiwa ni kinara kwa watupiaji na msimu uliopita alifunga mabao 23.

Kagere amesema:”Wananiita mzee sawa lakini nikiwa uwanjani ninawafunga wapinzani mabao jambo ambalo linamaanisha kwamba umri hauchezi mpira bali ni kipaji na juhudi ndani ya uwanja.

“Ninafurahia kufunga na wapinzani wangu wanalijua hilo ndio maana wamekuwa wakinikamia lakini ninawashinda kwa sababu mimi ni mchezaji wa kigeni ni lazima nionyeshe tofauti yangu na wao,”.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo imefunga mabao 63 imefungwa mabao 15 ikiwa na pointi zake 71.

Post a Comment

0 Comments