Katavi: Radi yaua watoto wawili na kujeruhi mmoja

Huzuni na vilio vimetanda kwa wakazi wa Mtaa wa Airtel na Nsemulwa kwa Mkumbo, Kata ya Uwanja wa Ndege wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi baada ya watoto wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka saba kupoteza maisha kwa kupigwa na radi.

Watoto hao walipigwa na radi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali, huku mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Hawa Jumanne akijeruhiwa kufuatia tukio hilo.

Akisimulia kwa masikitiko makubwa hali halisi ilivyokuwa, majeruhi wa tukio hilo Bi Hawa Jumanne amesema wakati mvua ikiendelea kunyesha alikuwa anakula chakula na mtoto wake ghafla alijikuta amerushwa nje na nguvu ya radi huku mwanaye akiwa anagalagala ndani ya nyumba kutokana na mshtuko wa radi hiyo.

Muuguzi Mkuu wa zamu katika hospitai teule ya rufaa Katavi, Bi Renata Kazungu ambaye amethibitisha kuwapokea watoto hao wawili wakiwa wameshapoteza maisha.

Post a Comment

0 Comments