Kiongozi wa upinzani aliyetekwa nyara nchini Mali anaendelea vizuri

Upinzani nchini Mali umesema kiongozi wake Soumaila Cisse anaendelea vizuri wiki moja tangu alipotekwa nyara na watu wasiojulikana na kwamba majadiliano yanaendelea kufanikisha kuachiwa kwake.

Chama chake cha URD kimesema tayari wamekamilisha malipo ya kumgomboa huku watu wengine nane waliotekwa pamoja wameachiwa lakini kiongozi huyo bado anashikiliwa.Cisse, waziri wa zamani wa fedha na mgombea wa kiti cha urais alichukuliwa kwa nguvu pamoja na wasaidizi wake kadhaa katika eneo lenye machafuko la katikati ya Mali baada ya watu wenye silaha kuvamia msafara wake.

Wakati wa kisa hiyo, mlinzi wa Cisse aliuwawa na watu wengine wawili walijeruhiwa na wapiganaji wanáodhaniwa kuwa wa kundi lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda linaloongozwa na muhubiri wenye msimamo mkali wa kidini Amadou Koufa.

Post a Comment

0 Comments