Makonda amtaka Waziri Kigwangala kuchapa kazi kuachana na mitandao

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ameingilia kati sakata la Waziri wa Maliasili Dkt Hamis Kigwangalla na wana-twitter, waliomzonga kufuatia ripoti ya CAG iliyobaini kuwa Wizara yake ilitumia Tsh Bil.2.58 kwa ajili ya kuanzisha chaneli ya TV ambazo hazikupitishwa na Bunge.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Makonda amemtaka Waziri Kigwangalla aendelee kuchapa kazi na aachane na masuala ya mitandaoni.

"Kaka yangu unajua ninavyokuthamini, chapa kazi achana na mitandao" ameandika Makonda.

Baada ya ripoti hiyo kubaini hivyo, CAG alitoa mapendekezo ya kwamba ni vyema Wizara ikahakikisha matumizi yote yanabajetiwa na kupitishwa na Bunge ili kuzuia utekelezaji wa shughuli za dharura, pia kuhakikisha marejeo ya bajeti zote yanapitishwa na Waziri wa Fedha na Mipango.

Post a Comment

0 Comments