Mambo yatakayokusaidia kuwa nafuraha katika maisha

Hakuna kiwanda ambacho kutengeza furaha isipokuwa mhusika mwenyewe kutambua jinsi ya kuwa furaha hiyo. Ni muhimu kufahamu namna ya kuwa na furaha kwa sababu furaha ni muhimu sana katika maisha ya kila mmoja wetu. Miongoni  mwa faida pekee itakanayo na furaha ni pamoja na kupunguza magonjwa yote yatokanayo na msongo wa mawazo.

Baada ya kusema hayo machache sasa naomba tuone mambo yatakayokusaidia kuwa na furaha kama ifuatavyo:

  • Usimchukie yeyote hata kama atakukosea sana.
  • Ishi maisha ya kawaida hata kama upo juu kimaisha.
  • Tarajia baraka hata kama magumu yanakusonga.
  • Toa hata kama wewe umenyimwa.
  • Onyesha tabasamu hata kama moyo unavuja damu.
  • Usiache kuwaombea wengine hata kama yako hayajajibiwa.


Endelea kutembelea blog hii pendwa  kila wakati. Asante.

Post a Comment

0 Comments