Marekani: Bernie Sanders abwaga manyanga


Mjumbe wa chama cha Democratic Bernie Sanders amejiondoa kwenye kampeni ya kuwania nafasi ya kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi wa rais wa nchini Marekani.
Sanders amewaambia wafuasi wake kwamba hatashiriki kwenye kinyang`anyiro cha chama cha Demokratic cha kumteua mgombea atakaepambana na Donald Trump katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.

Uamuzi wa Sanders unampa mshindani wake Joe Biden fursa ya kuwa mgombea wa pekee atakayepitishwa na chama cha Demokratic ili kupambana na rais Trump.

 Joe Biden aliyekuwa makamu wa rais wa Marekani katika utawala wa Barrack Obama alimzidi Bernie Sanders kwa jumla ya wajumbe mia tatu. 

Post a Comment

0 Comments