MICHEZO BeINSPORTS kupinga Newcastle kununuliwa na Bilionea wa Saudi Arabia

Kampuni ya BeINSPORTS yenye haki ya urushaji matangazo ya LIVE ya mechi za Ligi Kuu England (EPL), imetuma barua kwa vilabu 20 vya EPL ikiomba wapinge mpango wa Newcastle kuuzwa kwa Bilionea wa Saudi Arabia Prince Mohamed Bin Salman.
BeINSports imetuma barua hiyo ikidai kuwa kuuzwa kwa club hiyo kwa mtu kutokea Saudi Arabia kutashusha thamani ya Ligi ya EPL kwani Saudi Arabia inaoongoza kuonesha mechi za EPL za LIVE (Live Streaming) bila kuwa na kibali (Copy right).
Hata hivyo Newcastle haitakuwa club ya kwanza kumilikiwa na raia wa Saudi Arabia kutokea EPL, Sheffield United pia inamilikiwa na Bilionea Prince Abdullah bin Musa toka September 2019 kutokea Saudi Arabia.
Prince Mohamed Bin Salman ndio atakuwa bilionea mwenye utajiri mkubwa zaidi katika mabilionea wa EPL, utajiri wake ukitajwa kuwa zaidi ya Pound Bilioni 200.

Post a Comment

0 Comments