MICHEZO Corona: Uwanja wa wa Dortmund ulivyo tayari kutoa huduma

Club ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imeonesha wazi kuwa nia yao ya kutangaza kuwa uwanja wao wa Signal Iduna Park utatumika kama sehemu ya kutibia wagonjwa wa corona ilikuwa ya dhati.
Leo imeonesha maandalizi yalivyokamilika katika uwanja huo wakati huu Ligi mbalimbali duniani zikiwa zimesimama ikiwemo Ligi Kuu ya Ujerumani, sasa ni wazi Signal Iduna Park inaanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa corona.
Uwanja huo wa Iduna Park una uwezo wa kuingiza watazamaji 81,000 wakati wa mchezo, hadi sasa nchini Ujerumani visa vya corona vinatajwa kufikia 95,785, wamepona 15,072 vifo vikitajwa kufikia 1,431.

Post a Comment

0 Comments