MICHEZO Dybala aendelea kuteswa na corona wiki ya 6

Staa wa Juventus Paulo Dybala ameripotiwa kupimwa corona mara nne ndani ya wiki sita na kukutwa positive kwa mujibu wa kipindi cha El Chiringuito cha Hispania.
March 21 Dybala na mpenzi wake Oriana Sabatini walipimwa corona na kukutwa na maambukizi ya corona na kuanza kujitenga.
“Kwa Bahati nzuri tunaendelea vizuri siku hizi hatuna dalili zozote, nilikuwa na dalili kubwa nilikuwa nachoka haraka ninapotaka kufanya mazoezi, nashindwa kupumua baada ya dakika 5”>>> Dybala
”Tuligundua kuwa kuna kitu hakikuwa sawa na kupitia vipimo ambavyo club ilitufanyia tuliambiwa bado tuko Positive, kutokea hapo tulikuwa na dalili zaidi kama kikohozi, kuchoka na kusikia baridi lakini club toka ituambie kuwa tunaelekea kupona tunatakuwa kuwa nasubira”>>> Dybala
Hadi sasa ni wachezaji watatu wa Juventus ndio waliwahi kuripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona Blaise Matuidi, Daniel Rugan na Dybala.


Post a Comment

0 Comments