MICHEZO Eto’o na Drogba wakemea maprofesa wanaotaka kufanya majaribio ya kinga ya corona Afrika

Wakongwe wa soka wa Afrika waliojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa umahiri wao wa kucheza soka Didier Drogba kutoka Ivory Coast na Samuel Eto’o kutokea Cameroon wamekuwa wakali baada ya kusikia mpango wa madaktari wa Ufaransa wanaopambana kupata kinga ya virusi vya corona vinayosababisha homa kali ya mapafu.
Eto’o na Drogba wamepinga vikali kuhusiana na maprofesa wawili nchini Ufaransa ambao wamependekeza kuwa majaribio ya kinga ya corona (BCG vaccine) yaje kufanyiwa kwa watu wa Afrika, kitu ambacho kimetafsiriwa na wao kama ubaguzi wa rangi na kuwakosea heshima wa Afrika ambao ni binadamu kama walivyo wazungu.
Profesa Camille Locht kupitia moja kati ya vituo vya TV nchini Ufaransa “Kiukweli tunafikiria njia tofauti kiupana kufanya mafunzo Afrika kwa ajili ya kufanya majaribio ya BCG lakini haijatuzuia pia kufikiria kufanya majaribio haya ndani ya Ulaya na Afrika”
Eto’o
Staa wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o alionesha hasira zake baada ya kusikia hayo kupitia ukurasa wake wa instagrama kwa kuandika“Nyie ni Wa***, Afrika sio yenu kiasi cha kufikiria mnaweza kuichezea”
Kwa upande wa Didier Drogba ambaye amewahi kuichezea Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast kama nahodha aliandika kupitia twitter account yake “Haikubaliki kabisa kuendelea kukubaliana na hili kwa nguvu nakemea hili ubaguzi wa rangi na kuendelea kudharauliwa, tusaidieni kuokoa maisha Afrika na kuzuia kuenea kwa virusi ambavyo vitaenea dunia nzima, badala ya kutuchukulia kama nguruwe”


Post a Comment

0 Comments