MICHEZO Llorente ampa mbwa wake jina la uwanja wa Liverpool

Staa wa Atletico Madrid ya Hispania Marcos Llorente ameingia kwenye headlines baada ya kuamua kumpa jina Mbwa wake jina ambalo la uwanja wa Liverpool (Anfield).
Marcos ,25, jina hilo kampa mbwa wake ikiwa ni mwezi mmoja umepita toka Atletico Madrid waitoe na kuivua Ubingwa Liverpool katika michuano ya UEFA Champions League wakiwa katika uwanja wao wa Anfield.
Katika mchezo huo wa 16 bora uliyochezwa Anfield March 11 2020 na Atletico Madrid kushinda magoli 3-2.
Marcos Llorente alikuwa sehemu ya ushindi huo akifunga mgoli mawili dakika ya 97 na dakika ya 105 kabla ya Morata kufunga goli la mwisho dakika ya 120 na Liverpool kujikuta wakiondolewa kwa kipigo cha jumla (aggregate 2-4) hivyo Llorente inawezekana kamuita mbwa wake jina la Anfield kama sehemu ya kukumba historia aliyoiacha Anfield.

Post a Comment

0 Comments