Michezo Messi hajakubaliana na Jurgen Klopp kuhusu Mane

Nahodha wa FC Barcelona Lionel Messi ametoa kauli ambayo inapingana na kura ya kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kuhusiana na tuzo ya Ballon d’Or ambayo Lionel Messi aliibuka mshindi.
Messi aeleza kuwa anashangazwa kuona Sadio Mane wa Liverpool anamaliza nafasi ya nne katika tuzo hizo wakati alikuwa na msimu mzuri, akihojiwa na Canal + Messi alinukuliwa akisema.
“Ni aibu kumuona Mane anamaliza nafasi ya nne , nafikiri labda kulikuwa na kundi kubwa la wachezaji wazuri mwaka huu, ndio maana ikawa ngumu kumchagua, Mane amefanya makubwa sana na Liverpool ndio maana nimemchagua” >>>Messi
Kwa sasa inadaiwa kuwa Mane hana furaha Liverpool na yuko mbioni kuondoka baada ya kuona kuwa hata kocha wake Klopp alimpigia kura Van Dijk huku akiamini kwa kiwango alichokionesha alistahili kupata kura ya kocha hiyo  kwenye Ballon d’Or matokeo yalikuwa 1-Messi 2- Van Dijk 3- Ronaldo na 4- Mane

Post a Comment

0 Comments