Mmiliki wa klabu anayochezea Balotelli aigomea Serie A


Mmiliki wa klabu ya Brescia ya Ligi Kuu Italia (Serie A) Massimo Cellino ametangaza kuwa hawezi kuruhusu timu yake irudi uwanjani kumalizia msimu wakati huu wa corona.

Cellino anaamini msimu ni vyema ufutwe na yuko tayari timu yake iadhibiwe kwa kushushwa daraja Serie B, uamuzi bado haujawekwa wazi kama Ligi itaendelea au la.

Klabu ya Brescia ndio inayochezewa na mshambuliaji wa zamani wa Man City Mario Balotelli, hadi sasa Ligi Kuu ya Italia inatajwa kuwa itaendelea na kuna uwezekano zikachezwa mechi kila baada ya siku tatu huku ikidaiwa kuchezwa ukanda mmoja.

Post a Comment

0 Comments