Mzee Meshuku afariki akiwa na miaka 107, aacha wajukuu 300

Mzee Meshuku Mapi aliyeaga Dunia kutokana na maradhi ya uzee akiwa wa umri wa miaka 107, wake wanane watoto zaidi ya 50 na wajukuu zaidi ya 300, amezikwa katika viwanja vya Boma lake, ambapo baadhi ya waombolezaji wamemuelezea Mzee Meshuku kama shujaa wa maendeleo.

Mzee Meshuku maarufu kwa jina la Mzee Laibon alifariki Dunia Aprili 10 na alizikwa Aprili 15, 2020, katika Kijiji cha Esilalei ,huku wito ukitolewa kwa wanafamilia na jamii ya wafugaji, kumuenzi kwa kudumisha na kuendeleza yale yote aliyo kuwa ameyaanzisha.

Mzee Laibon katika hali isiyo ya kawaida kwa wazee wa umri na aina yake, alijiunga na Kanisa la KKKT na kubatizwa hii ikimanisha alifanikiwa kuwa muumini halali wa Kanisa hilo.

Post a Comment

0 Comments