S WHO: Hakuna chanjo ya corona itayofanywa Afrika

Baada ya kuwepo malalamiko dhidi ya kauli za kibaguzi za Madaktari wa Ufaransa, Shirika la Afya duniani (WHO) limesema Afrika haitofanyiwa majaribio ya chanjo ya virusi vya corona.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dr. Tedros ambae ni Raia wa Ethiopia, amekasirishwa na kauli hiyo ya kibaguzi iliyotolewa na Madaktari wawili wa Ufaransa waliokuwa kwenye kipindi cha TV waliotaka chanjo hiyo ifanyiwe majaribio Afrika pekee na sio sehemu nyingine duniani.
Dr. Tedros amesema Afrika haiwezi na wala haitokua uwanja wa majaribio kwa chanjo yoyote “imekasirisha na kusikitisha kuona karne hii kuna Wanasayansi wanatoa maoni kama hayo ya kibaguzi, tunawahakikishia hilo halitotokea”.
Kabla ya kauli hii ya WHO tayari Congo DRC iliripotiwa kukubali chanjo hiyo ikaanze kufanyiwa majaribio nchini humo kitendo ambacho kilipingwa na Watu mbalimbali wakiwemo Wakongwe wa soka Samuel Eto’o na Drogba

Post a Comment

0 Comments