TOP STORIES Meya wa Ubungo atangaza kung’atu Udiwani Ubungo

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob ametangaza kutogombea tena nafasi ya udiwani wa kata ya Ubungo katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020 nchini Tanzania.
Boniface Jacob ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika, “Nimetangaza kung’atuka ktk udiwani kata ya Ubungo muda wa madiwani utakapoisha, sitogombea tena udiwani uchaguzi ujao”
“Miaka 10 utumishi wangu ni kwa sababu Wana-Ubungo mlinikopesha imani. Tumekuwa wote wakati wa shida na raha, mabonde na milima.” Boniface Jacob
Hatua hiyo inakuja siku kadhaa baada ya wanachama zaidi ya 2000 wa chama chake kutia saini na kumfuata nyumbani kwake kumtaka agombee ubunge wa jimbo la Ubungo katika uchaguzi mkuu ujao 2020.

Post a Comment

0 Comments