Ufilipino yakataa kuwa China yatumia janga la COVID-19 kudhibiti Bahari ya China Kusini

     Serikali ya Ufilipino imepuuzia tahadhari leo kuwa China inatumia hali ya janga la virusi vya corona kupanua udhibiti wake katika Bahari ya China Kusini lakini nchi hiyo imeapa kulinda ardhi mipaka yake na haki ya uhuru wake.

Msemaji wa rais, Harry Roque , amesema serikali haikubaliani na mahitimisho yanayofanywa na baadhi ya wataalamu wa Ufilipino kuwa China inaongeza hali ya wasiwasi katika bahari hiyo katika wakati nchi zinajishughulisha zaidi na kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

Tangu Februari, China imekuwa ikipeleka meli, vyombo vya utafiti na meli za ulinzi wa pwani katika eneo hilo la kiuchumi la Ufilipino, Vietnam na Malaysia, katika hatua inayozidisha azma yake ya kuyachukua maeneo katika bahari hiyo, wataalamu wamesema.

Jaji wa zamani wa mahakama kuu ya Ufipino, Antonio Carpio, aliandika katika mtandao wa kijamii jana kwamba inasikitisha kwamba China inafanya hivi katika wakati huu wa janga la corona.

           

Post a Comment

0 Comments