Ujerumani yaituhumu Marekani kwa kutaifisha Barokoa

Ujerumani imeilaumu Marekani kwa kutaifisha maelfu ya Barakoa ambazo zilikwisha lipiwa na mamlaka za mji wa Berlin, na kusema hatua hiyo ni kitendo cha uharamia wa kisasa.

Waziri wa mambo ya ndani wa Berlin Andrea Geisel amesema maafisa wa Marekani walikamata shehena ya Barakoa 200,000 mjini Bangkok ambazo zilikusudiwa kutumiwa na Berlin katika kipindi hiki cha mripuko wa virusi vya corona.

 Jimbo la Berlin lilikuwa limeagiza Barakoa hizo kwa ajili ya maafisa wake wa polisi wanaoendelea kufanya kazi.

Wanasiasa wa Ufaransa pia hivi karibuni waliishutumu Marekani kwa kununua vifaa vya kujikinga ikiwemo barakoa kutoka China ambazo zilikusudiwa kupelekwa Ufaransa.

 Hata hivyo kampuni ya Marekani ya 3M imekana shutuma hizo. Serikali nyingi duniani hivi sasa zinategemea vifaa vya kimatibabu vya kujikinga kutoka China na wazalishaji wengine wa Asia.

Post a Comment

0 Comments